Kiungo wake Haruna Niyonzima.
Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
YANGA itamrudisha Rwanda kiungo wake Haruna Niyonzima kwenda kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR, hii ni baada ya juzi kuitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0 juzi.

Yanga ilishinda bao 1-0 likifungwa na Donald Ngoma ugenini, kabla ya
juzi mabao ya Amissi Tambwe na Thaban Kamusoko kuihakikishia nafasi ya
raundi ya kwanza.
APR, ambao walimuachia Niyonzima kutua Jangwani mwaka 2011 baada ya kuitumikia misimu minne, yenyewe ilifuzu kwa jumla ya mabao 4-2 mbele ya Waswaziland, Mbanane Swallow.
APR, ambao walimuachia Niyonzima kutua Jangwani mwaka 2011 baada ya kuitumikia misimu minne, yenyewe ilifuzu kwa jumla ya mabao 4-2 mbele ya Waswaziland, Mbanane Swallow.
Kwa mujibu wa ratiba, Yanga itaanzia ugenini Machi 12, mwaka huu kabla ya kurudiana Machi 19 jijini Dar. Mshindi kati yao, kuna uwezekano mkubwa akakutana na wababe wa Wamisri, Al Ahly ambao walikuwa wakisubiri mshindi kati ya Libolo ya Angola na Micomeseng ya Guinea ya Ikweta.
Mbali na Yanga, baadhi ya timu zilizofanikiwa kuvuka hatua hiyo juzi
Jumamosi ni Ferroviario Maputo ya Msumbiji iliyokuwa ikisubiri mshindi
kati AS Vita ya DR Congo na Mafunzo ambao ni wawakilishi wengine wa
Tanzania. Mchezo wa kwanza Mafunzo ilifungwa mabao 3-0 nyumbani.
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini sasa watakutana na Leopard ya Congo.
Timu nyingine zilizofuzu ni Warri ya Nigeria watakutana na Al-Merreikh
ya Sudan, Tripoli ya Libya na Al-Hilal ya Sudan huku St. Georges ya
Ethiopia wao watachuana vikali na mabingwa watetezi, TP Mazembe ya DR
Congo.
Timu nyingine zilitarajiwa kupatikana jana katika michezo ya marudiano.
Timu nyingine zilitarajiwa kupatikana jana katika michezo ya marudiano.

Note: Only a member of this blog may post a comment.