Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Stori: WAANDISHI WETU
DAR ES SALAAM: Mimba ya staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu
iliyokuwa gumzo kila kona, ni kama puto kwani baada ya kupulizwa, kujaa
na kuvuma sana, hatimaye limepasuka na kuacha vilio kwa familia na watu
wake wa karibu, Risasi Mchanganyiko linaweza kuripoti.
JIUNGE NA CHANZO
Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake ili kulinda
‘ushosti’ wake na Wema, kimeliambia gazeti hili kuwa mimba ya supastaa
huyo, ambayo inadaiwa kutojulikana mhusika halisi, imetoka baada ya
kuharibika muda mfupi tangu watoke kujiachia katika viwanja vya maraha
jijini Dar.
“Yaani ngoja nikwambie ukweli, ujue juzi hiyo kabla ya mimba kuharibika, tulikuwa naye kwenye sherehe yetu ya Timu Bella ambapo Wema alikuwa safi tu na cha ajabu siku hiyo hata hakunywa pombe kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.
HOSPITALINI AGA KHAN
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa hali ya Wema ilibadilika ghafla
baada ya kuanza kujisikia vibaya, ambapo tumbo lilianza kuuma na kumpa
maumivu makali ambayo yalisababisha damu kuanza kumtoka sehemu za siri,
jambo lililowafanya walio karibu naye kumkimbiza katika Hospitali ya Aga
Khan, Dar kwa matibabu.
“Alipofika kule ikafahamika kuwa ujauzito wake umeharibika,
kilichofanyika ni kumsafisha kama inavyokuwa kwa wajawazito wote
wanaoharibikiwa na mimba zao.”
IDRIS, WEMA WAANGUA KILIO
“Sijawahi kuwashuhudia Wema na Idris wakilia kwa uchungu kama
ilivyokuwa siku mbili hizi baada mimba hiyo kutoka, ni rahisi kwa watu
ambao hawajui hali halisi kuona kama Wema alikuwa akiigiza ila kama
ingetokea mtu wa nje angekuwa karibu kama ilivyo kwangu, wasingeweza
kumbeza kwa kumwambia hakuwa na mimba.”
Wema akiwa na mpenzi wake Idris.
MSIKILIZE MADAM MWENYEWE
“Kusema ukweli mimi kwa sasa sijisikii kuongea chochote juu ya hilo
maana hata kama nikiongea nini, ukweli utabaki kuwa mchungu kwangu, sipo
vizuri hivyo naomba niachwe kidogo, maana hakuna jambo jipya ninaloweza
kuliongea hapa likaeleweka zaidi ya kunyamaza,” alisema Wema.
BIBI KIKONGWE ATOBOA SIRI NZITO
Bibi mmoja kikongwe, Atha Magego (70) ambaye alikuwa mkunga enzi
zake, alisema kutoka kwa mimba ya Wema kumesababishwa na kelele nyingi
na kutotulia kwa mwanamke huyo maarufu.
“Vijana wa siku hizi hawajui miiko, mtu mjamzito hapaswi kuwa
mtembezi, hasa mbele ya watu wengi na mbaya zaidi usiku. Dunia ina watu
wengi wabaya, wanaweza kufanya lolote hata kama hawafaidiki.
“Kwa mtu maarufu kama Wema, hakupaswa kuwa mtembezi maana kuna macho mengi mabaya, angetulizana nyumbani na ikibidi angekwepa kabisa kuonekana ovyoovyo zaidi ya watu wake wa karibu. Lakini ukiacha hivyo pia, alipaswa kutulia nyumbani ili kuufanya mwili uzoee hali ya ujauzito,” alisema kikongwe huyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.