Kila mtu na mtoko wake,
mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athumani ‘King Majuto au Mzee Majuto’
anatengeneza mkwanja mrefu kwa kuwavunja mbavu watu.
Leo ndiye ana husika katika makala yetu ya utajiri na utapata kujua ni vitu gani anavyomiliki kupitia sanaa yake hiyo.
Mzee Majuto: “Kuna siri nyingi za
kufanikio lakini kubwa ni kutokubali kukatishwa tamaa hata kama kile
unachokipata ni kidogo. Ni kweli kupitia sanaa ya uchekeshaji nimepata
mafanikio lakini ni baada ya kupitia msoto mkali.
MASHAMBA
“Kwa kuwavunja mbavu watu, ninamiliki
mashamba yenye ukubwa wa heka 8 hivi. Pia nimeweza kusimama na kundi
langu la Majuto Unity lenye wasanii zaidi ya 50. Kwangu mimi haya ni
mafanikio makubwa.
MATANGAZO
“Nimekuwa mtu wa kujituma sana, ninafanya matangazo mengi ya bidhaa mbalimbali za chakula na mengineyo.
“Kwa upande wa magari nina Nissan Caravan, Toyota Hiace Custom, Noah na Kirikuu (Suzuki).
“Pia najishughulisha na ufugaji wa kuku, ng’ombe na mbuzi kama 20.
“Usisahau kwa kuchekesha watu, nina nyumba mbili zilizoko Tanga Mjini na nyingine kijijini kwangu.”
Huyo ndiye Mzee Majuto aliye wahi
kucheza sinema zaidi ya 70 za vichekesho zikiwemo Inye Gwedegwede,
Shikamoo Mzee, Ndoa ya Utata, Daladala, Nimekuchoka, Trouble Maker,
Kizunguzungu, Shoe Shine, Street Girl, Mtego wa Panya, Lakuchumpa,
Bishoo, Nakwenda kwa Mwanangu, Bishoo, Wizi wa Kuku, Mtu Mzima Hovyo na
nyinginezo.
Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 jijini
Tanga na kusoma Shule ya Msingi ya Msambwini jijini humo. Alianza
kuigiza akiwa na umri wa miaka 9 kwa kuigiza majukwaani. Pia ni mtunzi,
mwigizaji, mwimbaji na mwandishi wa miswada.
Hivi karibuni, Mzee Majuto alitangaza
kuacha kufanya kazi za wasanii wenzake kwa maana ya kushirikishwa na
kujikita zaidi katika kazi zake mwenyewe.

Note: Only a member of this blog may post a comment.