Flora Mvungi ‘H Mama’
Na Chande Abdallah
Msanii wa kike anayekipiga Bongo Muvi na
Bongo Fleva, Flora Mvungi ‘H Mama’ amefungukia madongo anayopigwa na
wasanii wenzake kuwa ameingia kwenye muziki kwa kubipu na kudai kuwa
bado yupo kwenye fani hiyo.
Akipiga mbili tatu na paparazi wetu, H Mama alisema kuwa anajiandaa
kuachia hewani ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mama Alisema
ambayo ina mahadhi ya mduara ili kuendeleza makali yake kwenye fani yake
ya muziki.
“Nani? Mimi siwezi kuacha muziki hao wanachekesha tu, hapa nilipo
naandaa ngoma yangu mpya nimeifanya kwenye Studio za Mo Fire,” alisema
Flora.

Note: Only a member of this blog may post a comment.