Msanii
wa muziki wa kizazi kipya ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa staili
yake ya kuimba kama mlevi, Michael Dennis Mhina ‘Joni Woka’ amefariki
dunia alfajiri ya leo Jumanne.
Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa
simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa Joni Woka amefariki katika
hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata
siku ya jana.
Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na rapper huyo kuelezea ajali hiyo:
Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na rapper huyo kuelezea ajali hiyo:
Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka, moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
Hii hapa ni moja ya video zake ziliwahi pata kutamba
Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.
Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family,
alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo,
ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.
Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.
Marehemu Michael Denis “John Walker” apumzike kwa Amani.


Note: Only a member of this blog may post a comment.