#UCHAGUZI2015:Kamishina wa Polisi, ACP Suleiman Kova amesema kuwa ameridhishwa na mwenendo wa kampeni za amani katika uchaguzi huu na kusema kuwa jeshi la polisi lipo mstari wa mbele kuhakikisha amani inatawala hivyo wananchi wasiwe na hofu,na kuwaasa watu wanao ingilia kazi ya tume kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya muda kupitia mitandao ya kijamii na sehemu nyingine kuacha kufanya mambo hayo na hatimaye waachie tume ifanye kazi yake hadi mwisho wa mchakato huu.
Hata hivyo ameipongeza ITV/Radio One na Capital Radio katika mchakato huu wa uchaguzi kwa kuonesha njia kama moja wapo ya kituo kikubwa nchini Tanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi ambapo watu wengi wanafuatilia kila kinachojitokeza sehemu mbali mbali za nchi.
Note: Only a member of this blog may post a comment.