Sunday, October 25, 2015

Anonymous

Rais KIKWETE: LOWASSA Ndio Mhusika wa Kashfa ya Richmond

Akiongea leo Mwanza kwenye kufunga kampeni za ccm Mh. JK amesema ni kweli alishiriki kwenye makubaliano ya kutafuta kampuni ya kufua umeme baada ya Mabwawa kukauka nchi, lakini hakushiriki kutafuta kampuni gani ilete umeme, hivyo hahusiki kwa namna yoyote kwa ujio wa Richmond.
Hivyo waziri Mkuu ndio mhusika mkuu wa Richmond! 
Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika na walikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .
By thehunk/JF

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.