Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma akisimulia kwa uchungu.
Mwandishi wetu
Hii ni habari ya kusikitisha! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma
anadaiwa kuteswa na kitu kilichoitwa pepo mbaya ambaye humsababishia
hasira kali hasa anapokosewa ambapo anapokumbwa na hali hiyo, hujikuta
anataka kuua.
TUJIUNGE NA CHANZO
Sosi aliye karibu na staa huyo aliyezungumza na Ijumaa mapema wiki
hii alinyetisha habari hiyo ambayo mbali na kumtesa Wastara, pia
inaitesa familia yake kwani mara nyingi huamua kukaa mbali naye pindi
anapokutwa na hali hiyo.Sosi huyo alinyetisha kwamba, kuna kipindi hali
hiyo ikimkuta Wastara huwa na stress (msongo) wa mawazo.
HARUFU YA DAMU, KUTAKA KUUA MTU
Ilidaiwa kwamba, akiwa katika hali hiyo, Wastara huunguruma kama mtu
aliyepandwa na kitu na husikika akisema kuwa anasikia harufu ya damu na
kwamba anataka kuua mtu.“Yaani unaambiwa hali hiyo ikishamtokea huwa
tunajifungia ndani na kumpisha anahangaika mwenyewe kwani tunahofia
jambo baya la mauti,” alisema sosi huyo ambaye ni mtu wa ndani ya
familia.
KUPOROMOSHA MATUSI
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kutaka kuua, pia
Wastara huporomosha matusi mfululizo ambayo akiwa kawaida hawezi
kuyatoa, kitendo kinachoshangaza, kwani anaweza kutukana kuanzia asubuhi
hadi jioni.
….Akizidi kusimulia.
BOFYA HAPA KUMSIKIA WASTARA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimwendea hewani
Wastara ili kujua kinachomsumbua ambapo alifunguka kwa masikitiko:
“Sijui ni nani amewafikishia habari hizi kwani zinanisikitisha sana
lakini naomba watu watambue kuwa nina tatizo ambalo sijajua nitalimaliza
vipi.“Wala huyo mtu hajakwambia uongo, ni kweli kwa sababu nina damu
mchanganyiko na nikikasirika nyumba nzima wanajifungia
ndani.“Ninajitahidi sana kujibadilisha ili niwe kawaida lakini
inashindikana. Ndiyo maana huwa napenda kukaa kimya sana kwani najijua
nina tatizo.
MCHANGANYIKO WA DAMU
“Nina mchanganyiko wa damu ya Kimasai, Kiarabu, Kinyamwezi, Kihindi,
Kinyarwanda na Kigunya ndiyo maana nahisi nina tatizo kubwa ambalo
naomba Mungu anitatulie.
“Kuna wakati huwa natamani kumpasua mtu pale anaponiudhi na asiamke kabisa ndiyo roho yangu inaridhika.
“Kuna wakati huwa natamani kumpasua mtu pale anaponiudhi na asiamke kabisa ndiyo roho yangu inaridhika.
Akiwa na simanzi.
ALA MARA TANO, SODA ISHIRINI KWA SIKU
“Ninapokuwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi huambatana na ‘stress’ zilizonizidi, huwa najikuta nakula sana kama mara tano kwa siku na huwa nakunywa soda kama ishirini hivi.“Mtu akiniona nanenepa ni kwa sababu ya stress za maisha ndiyo husababisha hali niliyonayo.
“Ninapokuwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi huambatana na ‘stress’ zilizonizidi, huwa najikuta nakula sana kama mara tano kwa siku na huwa nakunywa soda kama ishirini hivi.“Mtu akiniona nanenepa ni kwa sababu ya stress za maisha ndiyo husababisha hali niliyonayo.
AJITAHIDI KUSALI
“Huwa najitahidi kusali sana ili nione kama hali hii itaniondokea,
naamini ipo siku nitakuwa sawa na matatizo yote yataisha. Pia ni jambo
la kuombewa sana dua.
TUJIKUMBUSHE
Wastara amekuwa akikumbwa na mikasa ya kila aina kama ajali za mara
kwa mara hivyo kujiona mwenye mikosi ambapo mashabiki wake wamekuwa
wakimshauri kusali sana ili aepukane na mikosi hiyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.