Mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufu.
Richard Bukos, aliyekuwa Geita
Dk John Pombe Magufuli
ambaye ni mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekuwa gumzo kubwa katika maeneo
mbalimbali ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Katika ziara hiyo, wananchi walimpokea
kwa shangwe, vifijo huku wakionesha hisia zao wazi jinsi ambavyo
wanaamini Dk. Magufuli atafufua upya mwanga wa matumaini kwa wananchi
katika nyanja mbalimbali.
Mara kwa mara, watu walisikika mbele ya
mwandishi wetu wakisifu ahadi za Dk. Magufuli ambazo kwa hakika
zimeonekana kutekelezeka na kuwagusa moja kwa moja wananchi wa hali zote
za kimaisha.
Miongoni mwa ahadi ambazo zimegusa na
kukonga nyoyo za wakazi wengi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, ni pamoja na
kuboresha usafiri wa majini kwa kuongeza vyombo vya usafiri kwa njia
hiyo mfano meli, feri na pantoni, ambazo ni tegemeo kubwa kwa wakazi hao
kwa usafiri kutokana na mikoa hiyo kuzungukwa na ziwa Victoria.
Note: Only a member of this blog may post a comment.