Imelda Mtema
TAFRANI! Timbwili la aina yake liliibuka hivi karibuni Kiwalani Mivinjeni jijini Dar es Salaam kwenye mazishi ya kijana aitwaye Jackson mwenye umri wa miaka 28, baada ya dada yake kutaka kumpiga mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Monica, aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa marehemu akimhusisha na kifo hicho, Ijumaa lina mkasa kamili.
Habari kutoka msibani hapo zilidai kuwa, awali marehemu Jackson alikuwa ni mfanyabiashara wa ng’ombe na kwamba alikutana na Monica (38) mnadani huko Dodoma ambapo walishawishiana na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi uliowatoa huko na kuwaleta kuishi pamoja jijini Dar.
“Huyu dada anadaiwa alimshawishi kijana huyo waje waishi hapa na jamaa akaja akiwa na fedha za kutosha alizofanyia biashara baada ya kuwa amepewa mtaji na baba yake,” kilidai chanzo chetu msibani hapo.
Inadaiwa kuwa baada ya kufika mjini, walianza kuzitumbua fedha hizo taratibu hadi zilipoisha ndipo mizozo ya mara kwa mara baina yao ikaanza, kitu ambacho kijana huyo hakuridhika nacho kwani aliona kama anayenyanyapaliwa.
“Kijana huyo alikuwa akiumia sana wakati visa vilipokuwa vikiendelea, kwa sababu alijua asingeweza kurudi nyumbani kwao kwani fedha za mtaji alizopewa walishazimaliza, hivyo siku moja mwanamke huyo ambaye alikuwa muuza baa alipotoka, akaamua kujinyonga,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya Jackson kujinyonga, habari hizo zilisambaa haraka na kuwafikia ndugu zake ambao walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Inadaiwa kuwa songombingo lilitokea siku ya mazishi wakati Monica alipofika msibani kwani mwananamke mmoja aliyedaiwa ni dada wa marehemu alimfuata kwa lengo la kutaka ‘kumuanzishia’ akimtuhumu kuwa anahusika kwa na moja au nyingine na kifo cha mdogo wake.
“Yaani lilitokea timbwili, wakati padri akiendelea na ibada kulizuka ugomvi kati ya dada mmoja wa marehemu na mama huyo kiasi ambacho ilitumika hekima kuwatuliza ili shughuli ya mazishi iendelee,” alidai shuhuda huyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.