Mpambe wa staa wa Filamu Bongo, Wema Sepetu, Hamadi Manungwa ‘Petit Man’, juzikati alimuanika rasmi mrithi wa aliyekuwa mkewe, Esma Abdul ‘Esma Platnumz’ baada ya hivi karibuni kuingia kwenye mgogoro wa ndoa.
Baada ya gazeti hili kuanika habari ya kuvunjika kwa ndoa hiyo wiki
iliyopita huku Wema akitajwa kuwa chanzo ambapo yalizuka mambo mengi
mpaka watu kupelekana polisi, hivi karibuni Petit Man alimuanika
mwanamke mwingine akidai ndiye wa kuchukua nafasi ya Esma.
Esma kwa upande wake alisema anachosubiri ni talaka yake tu kwani
ameshachukua baadhi ya vitu vyake kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi na
Petit Man.

Note: Only a member of this blog may post a comment.