Producer wa Bongo Records, P-Funk Majani amesema muziki wa Bongo
Flava sasa umegeuka kuwa miongoni mwa vitu vinavyoheshimika zaidi
nchini.
Akiongea na kituo cha runinga cha Azam Two kwenye hafla ya wasanii
kumuaga Rais Jakaya Kikwete, Majani alisema zamani heshima haikuwepo
kabisa.
“Sasa hivi kila mtu anaitambua Bongo Flava na anaikubali,” anasema Majani.
“Hata pia viongozi wetu zamani walikuwa kidogo wakisikia kuhusu
muziki wanaona kitu cha uhuni au nini. Imeonekana ni biashara, makampuni
pia yamekuja yamejitokeza yanawekeza kwenye muziki,” ameongeza.
“Wasanii wenyewe wameongezeka. Pia tumeweza kupanua mipaka yetu, sasa
hivi tunasikika Afrika nzima so haya ni mafanikio makubwa. Teknolojia
pia imesaidia lakini kwa ufupi watu wameanza kusupport muziki wao,
kuupenda na kuuthamini.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.