Tuesday, August 11, 2015

Anonymous

KUFURU! Tyga amnunulia mpenzi wake Kylie Jenner gari la shilingi milioni 665 kama zawadi ya birthday

Usiseme hatuna hela, sema huna hela!
kylie-birthday-9-435 Ferrari: Zawadi ya birthday ambayo Kylie amepewa na mpenzi wake Tyga
Katika kuhakikisha tabasamu kwenye uso wa mrembo wake Kylie Jenner halikauki, rapper Tyga amemsurprise kwa kumnunulia gari aina ya Ferrari 482 Italia yenye thamani ya $320,000 ambazo ni zawadi ya shilingi milioni 665!
kylie-birthday-1-435  
Tyga akimkabidhi Kylie ufunguo wa gari alilozawadiwa na kumwacha mdomo wazi
Kylie Jenner ametimiza umri wa miaka 18 Jumatatu hii.
Kwa mujibu wa mtandao wa People, Tyga alimpa mpenzi wake gari hilo lenye rangi nyeupe kwenye sherehe iliyofanyika huko West Hollywood iliyohudhuriwa na mastaa kibao.
kylie-birthday-7-435
Mastaa waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Kim Kardashian, Kanye West, Khloe, Kourtney, Kendall, Kris na Caitlyn Jenner.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.