Kocha wa klabu ya Manchester City ya Uingereza Manuel Pellegrini ana matumaini ya kupona kwa kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure ambae alikuwa na wakati mgumu msimu uliopita hivyo anaimani Yaya atafanya mambo mazuri msimu huu.
Pellegrini ana amini Yaya Toure
hastaili lawama alizozipata msimu uliopita hivyo huu ni wakati wake wa
kufanya vizuri. Kwa mujibu wa wakala wa kiungo huyo alimwambia Pellegrin kuwa Yaya hakuwa na msimu mzuri kutokana na kupata matatizo ikiwemo kufiwa na mdogo wake.
“Tuliongea
kabla ya kuanza kwa msimu na uhakika tutamuona Yaya Toure kama wa miaka
miwili iliyopita, ni mchezaji muhimu kwetu, Sifikirii kama Yaya
anastahili kupata lawama kama alizozipa msimu uliopita, ni mchezaji
muhimu kwetu ila ni ngumu kufanya vizuri kama utakuwa na matatizo
”>>>Pellegrini
Kocha huyo ana amini Yaya
hakufanya vizuri msimu uliopita kutokana na matatizo ikiwemo kufiwa na
mdogo wake ambae alikuwa mchezaji pia lakini hadi mauti una mkuta
alikuwa katika Jiji la Manchester.
Note: Only a member of this blog may post a comment.