Pazia la ligi kuu ya England limefunguliwa leo rasmi kwa mchezo wa
kugombea taji la ngao ya hisani ya FA – mechi ambayo inawakutanisha
washindi wa kombe la Barclays Premier League na mshindi wa kombe la FA
au League Cup.
Mchezo wa Ngao ya hisani mwaka huu umewakutanisha mahasimu wa jiji la London – Chelsea dhidi ya Arsenal, na matokeo ya mchezo huo ni ushindi kwa vijana wa Arsene Wenger.
Pia siku ya leo imekuwa nzuri kwa kocha Wenger ambaye leo ndio mara
ya kwanza ameweza kupata ushindi dhidi ya timu anayoiongoza Jose
Mourinho.
Ligi kuu ya Uingereza itaanza rasmi wikiendi ijayo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.