Wakati
ambapo vyama vya upinzani vinatarajia kuzindua kampeni zake katika
uwanja wa Jangwani kesho na kumnadi mgombea wake wa urais, Edward
Lowassa, duru zinaeleza kuwa huenda Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad
Slaa akahudhuria uzinduzi huo.
“Zipo taarifa za chinini kuwa Dk. Slaa atahudhuria uzinduzi, hatujui zina ukweli kiasi gani na atashiriki kama Katibu Mkuu au mgeni mwalikwa, kama atahudhuria, atatusaidia sana na asipokuja suala lake litaendlea kuwachanganya wafuasi wa Chadema,” alinukuliwa kiongozi huyo wa Chadema.
Haijafahamika kama taarifa hizo ni za kweli au la kwa kuwa hata uamuzi wa kumkaribisha Edward Lowassa kujiunga na Chadema ulifanywa kuwa siri kubwa kwa viongozi wachache sana takribani miezi mitatu kabla. Hata viongozi wengine wa ngazi za juu walikuwa hawajui kabisa kinachoendelea.
Dk. Slaa alijiweka kando na harakati za kampeni za Chadema na Ukawa kwa ujumla baada ya kutoridhia uamuzi wa chama chake kumkaribisha Edward Lowassa ambaye awali walikuwa wanamtuhumu kuwa katika orodha ya mafisadi wakubwa nchini.
Ukawa wanatarajia kufanya uzinduzi wao kesho (Agosti 29) katika viwanja vya Jangwani ikiwa ni wiki moja baada ya CCM kuutumia uwanja huo kwa shughuli hiyohiyo.


Note: Only a member of this blog may post a comment.