Gladness Mallya na Hamida Hassan
WAKATI
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukielekea ukingoni, staa wa filamu Bongo,
Salma Jabu ‘Nisha’ amekwea pipa kuelekea nchini China akidaiwa kumfuata
bwana wake kwa ajili ya kwenda kufanya maandalizi ya Sikukuu ya Idd.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa Mwalumu Julius Kambarage Nyerere.
“Hivi hamjui kwamba Nisha sasa hivi mambo yake ya kifedha siyo mabaya
kwani ana mpenzi mwenye hela sana anaishi China na ndiye amemwita huko
japokuwa anawadanganya watu kwamba anaenda kufanya filamu, leo (Jumanne
iliyopita) nasikia anasafiri muwahini Air Port,” kilisema chanzo hicho.

Note: Only a member of this blog may post a comment.