Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Zaituni almaarufu Zai,
mkazi wa Tandika, Dar, ambaye ni mke wa mtu amejikuta akila kibano
‘hevi’ baada ya kunaswa laivu kwa wizi wa madela madukani.
Zaituni anayedaiwa kuiba madela.
Tukio hilo linadaiwa kuchukua nafasi hivi karibuni kwenye maduka ya
Kariakoo jijini Dar ambapo Zai akiwa na mwenzake aliyemtaja kwa jina
moja la Maimuna waliwelewa mtego baada ya kushtukiwa mchezo wao huo.
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, Zai na mwenzake waliingia kwenye duka
moja ambapo wafanyabiashara wanaoujua mchezo wao walimtonya mwenye duka
ambaye alianza kuwafuatilia.
Ilielezwa kuwa wakiwa ndani ya duka hilo, wanawake hao walianza
kuchikichia madela kwenye mikoba yao lakini Maimuna aliposhtuka kuwa
mwenye duka anawachora ndipo akatoka nduki huku akimwacha Zai
aliyejikuta akiwekwa chini ya ulinzi na wafanyabiashara hao.
Wakati wakisubiri polisi wafike eneo la tukio, jamaa hao walimpa Zai kibano cha uhakika ambapo alikuwa akijitetea:
“Jamani mimi siyo mwizi nimeponzwa na mwenzangu anaitwa Maimuna.
“Kwa hapa Dar ninakaa Tandika, ni mke wa mtu. Nimeolewa na nina watoto wawili, Bakari na Rashid. Mume wangu hana kazi.“Mwenzangu ndiye ameniambia tuibe madela. Huwa anakwenda kuyauza mikoani tunagawana hela. Yeye anachukua nyingi na mimi kidogo.
“Naombeni msinipele polisi kwa sababu sijawahi kupelekwa huko.”
Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, wafanyabiashara hao waliendelea kumshikilia Zai huku wakisisitiza lazima akakae nyuma ya nondo kisha sheria ichukue mkondo wake kwani kumekuwa na wimbi la wizi wa vitu madukani unaofanywa na baadhi ya wanawake wasiokuwa na kazi mjini.

Note: Only a member of this blog may post a comment.