MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amedai kuwa ‘Bongo
Movies’ wameharibu sanaa ya uigizaji hapa Tanzania. Nora amefunguka
hayo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa Instagram mara baada
ya kuweka picha hiyo hapo juu akiwa lokesheni wakishuti movie.
"Naipenda kazi yangu na ninaiheshim sanaaaaa hii ndo
sanaa ilionikuza mpaka leo na bado nakua nayo Mungu afungue heri zake
lol tunajua kukomaaa ila nais Mungu ndo ameandika.
Nitatumia kipaji changu akili yangu kuwatumikia
Watanzania pale palipokua apajaenda sawa nawaakikishia hiii kitu
imewabeba wooooootee kiasi kwamba utatamani kumwita mama yako mnakaa
mnajifunza kitu unakaa na baba yako mnaangalia sio kama movie nyingi
zilizopo hukai na wazazi wako mkaangalia mana unajua wataharibu tuuuuu
ila hii sio movie manaa bongo movie wamesharibu sanaa ya uigizaji
tanzania," Nora ameandika.
Una maoni gani juu ya mtazamo huu wa Nora?

Note: Only a member of this blog may post a comment.