Hans Mloli,Dar es Salaam
SIMBA wanajua kuwa wakifanya mchezo katika nafasi ya straika, basi msimu ujao watafulia zaidi.
Ili kuonyesha hawataki utani wameamua kusaka straika wa uhakika katika nchi tano ikiwemo Senegal pamoja Ghana kwa upande wa Afrika Magharibi.
Pamoja na nchi hizo mbili, Simba wataendelea kusaka mshambuliaji mkali katika nchi za Burundi, Kenya na Uganda ili kupata mmoja ambaye atapewa jukumu la kuisaidia Simba kupata mabao.Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema nchi walizopanga kusaka mchezaji ndiyo hizo.
“Tunaamini tunaweza kupata straika mzuri mwenye uwezo wa juu katika nchi tano ambazo tuna imani nazo katika nafasi hiyo, tunaangalia katika nchi za Burundi, Kenya, Senegal, Ghana na Uganda. Lengo ni straika mmoja, tukimaliza hapo tutakuwa na wachezaji wageni wanne na hiyo nafasi moja tutaangalia kama kutakuwa na usajili wa nafasi yoyote ya lazima,” alisema Hans Poppe.
Simba imeamua kuachana na Waganda Dan Sserunkuma na Joseph Owino na kuwabakiza watatu ambao ni Emmanuel Okwi, Simon Sserunkuma na Juuko Murshid.
Mpango wa Simba ni kuziba nafasi zote mbili za wageni kwa kusajili washambuliaji na moja inamuangukia Mkenya, Kiongera.Hiyo moja pia nafasi bado inaonekana iko kwa Mrundi, Laudit Mavugo (pichani mbele) aliyetamba na Vital’O ya kwao Burundi pia Polisi ya Rwanda wakati huo ikinolewa na Goran Kopunovic.
Mavugo ameonyesha kuwavutia zaidi Simba, hivyo kama hawataridhika na washambuliaji wanaotaka kuwasajili katika nchi za Senegal, Ghana na Uganda basi Mrundi huyo ndiye atapewa nafasi ya kumaliza kazi ya ‘kuchana’ nyavu za wapinzani.
Iwapo Mavugo atatua, maana yake atapewa nafasi ya kushirikiana na Kiongera na mzalendo, Ibrahim Ajibu pamoja na Okwi kuhakikisha Simba inakuwa tishio.
Simba inahangaika kusaka mshambuliaji kutokana na kumuachia kimakosa Amissi Tambwe kwenda Yanga. Tambwe alikuwa mfungaji bora Tanzania 2013/14 baada ya kufunga mabao 19 lakini alipoenda Yanga moto wake umeendelea kuonekana kufuatia kufunga mabao 11 ya ligi pamoja na mengine muhimu ya kimataifa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.