Hii nyingine kutoka Bungeni pia leo Dodoma, kukawa na mvutano baada ya Mbunge Felix Mkosamali kumhusisha Rais na kushindwa kwa mapambano ya Rushwa.
>>Kwanini
Taasisi mbalimbali ziwe chini ya Rais? Kwanini TAKUKURU iwe ofisi ya
Rais na isiwe chini ya Waziri Mkuu… Hizi Taasisi za Ofisi ya Rais ndio
zina njaa kwelikweli.. ukiona TAKUKURU inafeli maana yake Rais hana
utashi wa kisiasa wa kupambana na Rushwa.. Awamu ya nne imeshindwa
kupambana na Rushwa, mnakusanya kodi hamna uwezo wa kutekeleza vitu hivi” >> Mbunge Felix Mkosamali.
Akasimama Waziri Mkuchika >> “Kwa
mujibu wa kanuni inayosema Mbunge hatotumia jina la Rais kwa dhihaka
katika mjadala au kwa madhumuni ya kulishawishi Bunge.. Mkosamali
ameeleza Rais hana utashi wa kisiasa wa kupambana na Rushwa..
Kiustaarabu afute tu hiyo kauli>>
Mkosamali akaendelea >> “Nitafutaje wakati ndio hali halisi.. Juzi Katibu Mkuu amesafisha watu.. Kesi zote zikichunguzwa DPP anazifuta mbona yako wazi”>>
Akasimama Mbunge Innocent Sebba >> “Niwashukuru
Mawaziri wanaohusika na Ofisi ya Rais.. Pamoja na kelele zinazopigwa
hawa wenzetu tunawaita ni wapiga debe sio wasafiri.. Wanaosafiri wanajua
wanakoelekea.. msikate tamaa kwa ajili ya hawa wapiga debe”>>
Baadae akapata nafasi Waziri Mark Mwandosya >> “Hoja
ya leo inamzungumzia Ofisi ya juu kabisa katika nchi.. unapokizungumzia
chombo hiki kipe heshima inayohitajika.. Huwezi ukamzungumzia Rais kama
unavyomzungumzia Mbunge wa Rungwe“>>
Sikiliza live hapa chini...
Sikiliza live hapa chini...
Note: Only a member of this blog may post a comment.