Jana ilikuwa headlines za mgomo wa
wanafunzi Chuo Kikuu Dar, leo imesikika ishu ya kutaka kuibuka mgomo na
maandamano Iringa na Polisi wakaingilia kati.
Hii leo ilikuwa Bungeni Dodoma, swali kutoka kwa Mbunge Esther Bulaya; >>“Jana
wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wamegoma sababu hawakupelekewa
fedha za kujikimu.. wanafunzi wengi wanatoka maeneo ya vijijini watoto
wa maskini, Chuo Kikuu cha Saint Joseph wameamua kuwarudisha wanafunzi
wa mwaka wa kwanza kwa sababu ya kukosa fedha.. Tunahitaji majibu ya
Serikali kwa nini hawapeleki fedha za kujikimu kwa wanafunzi mpaka
wanafunzi wagome?”>>
Majibu ya Naibu Waziri Mwigulu Nchemba >> “Niwaombe
radhi wanafunzi wa vyuo vikuu.. Tuliongea na viongozi wa vyuo pamoja na
bodi na Wizara inayosimamia, kulikuwepo na utaratibu wa kuipa fedha
hizo na mpaka jana tayari fedha ilishatoka Wizara ya fedha.. wataalamu
ambao wanashughulikia kuzifikisha hizo fedha kwa wanafunzi watoe kwanzaq
fedha hizo ndio wakae vikao kuliko kusubiri kupitisha kwa utaratibu
ambao wanafunzi wataendelea kupata shida”>>
>>“Serikali
tunajitahidi kuhakikisha kwamba tunawafikishia kwa wakati fedha..
Serikali imeshatoa fedha na taasisi zinakopita wajitahidi leo leo vyuo
vyote viwe vimeshapata fedha hizo”>> Naibu Waziri Mwigulu Nchemba.


Note: Only a member of this blog may post a comment.