Baadhi ya watu jana mchana ‘waligida’
pombe za bure baada ya Fuso lililokuwa limebeba masanduku ya bia
kupinduka katika Barabara ya Mandela, Dar es Salaam baada ya Fuso hilo
kugongwa kwa nyuma na lori na kupinduka.
Kundi hilo la vijana hao wakiwemo
madereva wa bodaboda walivamia na kuchukua chupa za bia na kunywa huku
wengine wakinywa mfululizo.
Tukio hilo lilidumu kwa takribani 20 kabla ya polisi kuongeza nguvu.
Vijana wengine waliingia mitaroni ambako
bia ziliangukia na kuzichukua bila kujali kuwa zimepasuka, muda mfupi
baadae wengine wakaanza kulewa.
Dereva wa Fuso hilo Mohamed Said alisema mzigo huo wa bia aliutoa katika Kiwanda cha Serengeti kwenda Kituo cha Polisi Mkoa wa Pwani.
“Hizi bia
zilikuwa katika masanduku 500 ni mali ya Polisi Pwani, ajali hii ni
uzembe unaoonekana wazi kuwa wa dereva wa lori, hata polisi wakija
kupima watajua nani mwenye kosa,” alisema Said kabla ya Fuso lingine kufika na kuchukua bia hizo na kuondoka nazo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema chanzo
cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akitokea njia ya
pembeni kuingia barabara kuu bila tahadhari japo dereva wa lori amekataa
kusababisha ajali hiyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.