Wednesday, April 1, 2015

Anonymous

MATUSI, NGUMI ZATAWALA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR



Wajumbe wa baraza la wawakilishi wameweka tofauti za seriklai ya kitaifa pembeni na kuanza kutupiana matusi na kutishia kupigana hadharani ndani ya baraza baada ya mabishano kuhusu hoja ya vitambulisho vya Zanzibar.

Hali hiyo ambayo haijawahi kutokezea ndani ya baraza hilo ilianza wakati wajumbe walipokuwa wakianza kuchangia hoja hiyo binafsi ya mwakilshi wa CUF Mh. Hamad Masoud ambapo mwakishi wa CUF jimbo la magogoni Mh. Abdillahi Jihad ambaye pia ni waziri alipaonza kumshambulia wazir wa nchi tawala za mikoa na idara maalum Mh. Haji Omar Kheir.

Hapo ndipo sakata hilolilipoanza ambapo naibu waziri amabye ni CCM Mh. Haji Gavu alipaona kukwaruzana kwamaneno na matusi dhidi ya mwakilishi wa CUF na kutaka kugeuza ukumbi huo kuwa wa masumbwi.

Pamoja na jitihada za spika Mh. Pandu Ameir Kificho kutaka kuwepo kwa amani na utaratibu hakiusaidii lolote na fujo hizo zikageuka kwa wawakilishi wa CCM Mh. Hamza Hassan Juma na mwakilishi wa CUF Mh. Salum Nassor ambao mnao wataka kuzipiga na kutishiana kwenda nje.

Hili ni tukio la pili kutokea ndani ya mkutano huu wa baraza ambao wawakilishi wa CUF na CCM kuvutana na kubishana kwa maneno ya matusi na kejeli.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.