Friday, April 24, 2015

Anonymous

MADAKTARI WAGEUKA MADEREVA BAJAJI DODOMA

Madaktari wageuka waendesha bajaj za wagonjwa baada ya kukosekana kwa madereva mkoani Dodoma. Madaktari katika maeneo yaliyonufaika na bajaji za kubeba wagonjwa , wamelazimika kuwa madereva wa kuziendesha baada ya serikali kutoajiri madereva.

Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk Ezekiel Mpuya aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza ofisini kwake mjini hapa.
Alisema mkoa wa Dodoma ulifanikiwa kupata bajaji 10 na kila wilaya ilipatiwa bajaji mbili.
“Tuligawa bajaji mbili kwa kila wilaya kipindi kile kabla ya kuongezeka kwa wilaya ya Chemba, lakini zote hazina madereva,” alisema.


Dk Mpuya alisema madaktari hao licha ya kuziendesha bajaji hizo, hukumbana na changamoto za ubovu wa barabara unaowapa wakati mgumu pindi wanapowasafirisha wagonjwa wanaowapatia rufaa ya kwenda Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
“Wakati mwingine huwa zinafia njiani kutokana na ubovu wa barabara, kwa upande mwingine naweza kusema sio msaada sahihi,” aliongeza. 


Ameiomba serikali kutazama uwezekano wa kuzipatia magari ya wagonjwa hospitali hizo ili kuepuka adha wanayokumbana nao sasa.
Chanzo: Mwananchi

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.