KIMEELEWEKA! HATIMAYE MWENYEKITI WA WAFANYABIASHARA AACHIWA KWA DHAMANA DODOMA
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, (mwenye koti la
kahawia), akisindikizwa na mawakili na wafanyabiashara wenzake.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja
ameachiwa kwa dhamana leo jijini Dodoma baada ya kushikiliwa kwa siku
sita kufuatia kuondolewa dhamana ya awali kwa madai ya kukiuka masharti
ya dhamana.
Minja ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa
Dodoma ikiwa ni siku moja baada ya suala lake kuibuliwa bungeni mjini
Dodoma kwa baadhi ya wabunge kuitaka serikali kukaa na kuangalia namna
ya kuweza kumaliza mgogoro uliopo kwa kupatiwa dhamana kwa mwenyekiti
huyo.
Kushikiliwa kwa Minja kumesababisha kuwepo migomo ya wafanyabiashara
katika maeneo mbalimbali nchini waliokuwa wamefunga maduka yai
kushinikiza kuachiwa kwa mwenyekiti wao huyo.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
KITAIFA
on Wednesday, April 1, 2015
Note: Only a member of this blog may post a comment.