Sunday, April 5, 2015

Anonymous

KARDINALI PENGO ATOA KAULI TATA MADAI YA KUTUMIKA NA CCM KUHUSU KATIBA

Mwadham Cardinal Pengo akitoa maelezo juu ya sakata linaloendelea juu ya mchakato wa katiba amesema yeye hatumiki na CCM katika maswala ya katiba. Askofu Pengo amehoji juu ya shutuma ambazo wengi wanamzungumzia kama yeye anatumika na CCM. Je, wanaompinga wanatumika na UKAWA? 

Suala hili limezuka baada ya Askofu Pengo kuenda kinyume na msimamo wa maaskofu wa kikristu ambao walitoa tamko kwamba wananchi waipigie kura ya hapana katiba inayopendekezwa kutokana na sababu ya kuwepo kwa mchakato wa kuingizwa kwenye katiba hiyo suala la mahakama ya kadhi.

Kutokana na msimamo huo Askofu Pengo alitoa tamko tofauti na msimamo wa maaskofu wenzake kwa kusema kwamba viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwaamlia wananchi au waumini kupiga kura ya hapana bali wananchi au waumini wanatakiwa kuachwa huru kuamua wenyewe kupiga kura ya hapana au ndiyo kwa kadri ya utashi wao

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.