Mahakama ya wilaya ya Tabora imehukumu Masudi Nassoro mkazi wa kata ya Kiloleni manispaa ya Tabora (20) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya ulawiti kwa mwanafunzi wa kike wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 9.
Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Tabora mjini,Bahati Chitepo amesema kwamba ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia kama hiyo kwa watoto, na jamii ijifunze kutoka kwake.
Awali mwendesha mashitaka wakili wa serikali Miradi Kijulu amesema kuwa mshitakiwa Masoud Nasoro alitenda kosa hilo eneo la kata ya Kiloleni ambapo muathirika wa tukio hilo alimuomba lifti akiwa anakwenda shuleni na ndipo mshitakiwa alimpeleka vichakani mtoto huyo eneo la Kalunde na kumfanyia unyama huo.
Baada ya kutenda kosa hilo mshitakiwa alikimbia hadi alipotiwa nguvuni na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo mshitakiwa huyo aliiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwani anaishi na babu yake mlemavu wa mguu na wazazi wake wote wamafariki dunia, maombi ambayo yaliyupiliwa mbali.
Via>>ITV

Note: Only a member of this blog may post a comment.