Sunday, March 22, 2015

Anonymous

KIMENUKA SIMBA SC: RAIS AMPA KOPUNOVIC DAKIKA 630!

Na Khadija Mngwai, Dar es Salaam.
RAIS wa Simba, Evans Aveva, ametoa maagizo mazito kwa benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na Mserbia, Goran Kopunovic kuhakikisha wanashinda michezo yote iliyo mbele yao. 

Mabingwa hao wa zamani wa Bara, wamebakiwa na michezo saba kabla ya kumaliza msimu huu ambayo ni sawa na dakika 630. Simba ipo nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu kwa kuwa na pointi 29 nyuma ya Azam yenye pointi 33 na Yanga yenye 34. 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Aveva alisema kuwa moja ya mikakati waliyojiwekea ni kuhakikisha wanashinda michezo yote iliyobaki “Kwa sasa hatutazami suala la ubingwa wa ligi msimu huu ila tunachotaka ni kuweza kushinda michezo yetu yote iliyobakia na tayari nimeshatoa maagizo katika benchi la ufundi kwa ajili ya utekelezaji.
“Tunahitaji kumaliza katika nafasi nzuri, hivyo ni lazima tufanye vyema katika mechi zilizobakia bila kupoteza,” alisema Aveva.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.