Wednesday, April 1, 2015

Anonymous

KIFO CHA ABDU BONGE MMOJA MBARONI

Issa Mnally Na Richard Bukos 
MWANAMKE mmoja anashikiliwa na polisi kufuatia kifo chenye utata cha aliyekuwa meneja wa kundi la muziki wa kizazi kipya la Tip Top Connection, Abdul Shaaban Taletale, maarufu kama Abdul Bongo kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. 

Marehemu Abdul Bonge alikutwa na umauti Jumamosi iliyopita huko Magomeni Kagera alikokuwa akiishi baada ya kuitwa kwenda kusuluhisha ugomvi kati ya mtu mmoja anayeitwa Nassoro Idd na mkewe. 

Anayeshikiliwa ni mke wa Nassoro (jina halikufahamika mara moja) baada ya mwanaume huyo kudaiwa kukimbilia kusikojulikana, kufuatia Bonge kukutwa ameanguka ndani ya chumba cha wawili hao waliokuwa katika ugomvi na haijafahamika hadi sasa ni kipi hasa kilimsibu meneja huyo, mmoja wa watu muhimu katika tasnia ya muziki nchini. 

Baada ya kukutwa chumbani hapo akiwa hajiwezi, marehemu alikimbizwa katika Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese Darajani, ambako inadaiwa madaktari walithibitisha alifariki dunia. Mwili wake ulipelekwa Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi. 

Baada ya uchunguzi huo, inadaiwa polisi walihitaji kujiridhisha zaidi, hivyo Jumapili iliyopita mwili huo ulihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi ambayo yalitarajiwa kufanyika mkoani Morogoro mapema wiki hii.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.