Kangi Lugola, Yusuph Salim na David Silinde ni baadhi ya Wabunge waliochangia muswada huo;
“Tatizo
kubwa la kwanza kabisa waheshimiwa wabunge ni tabia ya kulindana
kuwalinda wafanyabiashara ambao ndio wanafanya biashara za madawa ya
kulevya, ni kweli wanafahamika kwa majina na mahali wanapoishi.
Lakini
kwa sababu tumeamua kuwalinda kwa sababu na sisi tunanufaika hatutaki
kuweka mamlaka wakati bado tabia hii ya kulindana tunayo tatizo la
madawa ya kulevya halitaondoka katika nchi yetu, Jeshi la Polisi pale
wakimkamata mfanyabiashara wa madawa ya kulevya simu za wakubwa
zinapigwa wanawaacha akipelekwa mahakamani kumejaa rushwa kesi haziendi
wanamuachia“– Kangi Lugola.
“Leo Wabunge tunataka kumchomekea Kangi ataje wakati waliowahi kutaja na kupambana na watu hawa hata walipopoteza maisha hawakumbukwi, Kangi Lugola tunampenda au hatumpendi jamani?“
Tunajadili
vitu ambavyo uwezo wetu wa kukabiliana navyo unaonekana dhahiri ni
mdogo tunavyozungumzia dawa za kulevya tunazungumzia sehemu yenye watu
wenye nguvu watu wenye fedha watu wenye uwezo wa kumfanyia mtu kitu
chochote na wasifanywe chochote“
“Vyombo vya habari ushauri wangu
visingetaja thamani ya madawa.. ni bora vingetaja athari lakini vikataja
na adhabu anayotakiwa kupewa. Ukiitangaza ile adhabu kwamba madawa
aliyokutwa nayo adhabu yake ni kunyongwa mpaka kufa wote watakaoiona
hiyo taarifa halafu wakaona asubuhi kanyongwa watu wataogopa…”–Mbunge Livingstone Lusinde.
“Uangalie
tena sasa familia ya yule kijana ambae anatumia madawa ya kulevya namna
ambavyo imeathirika kiuchumi imefilisika kwa sababu vijana wale
wanaadhiri familia zao wanaharibu kila kitu ndani za familia zao“
Wakati
mwingine wanaiba mpaka vikombe ili auze apate unga, athari ambayo mtu
mwenyewe anapata, athari ambayo familia ya kijana mla unga anaipata kwa
sababu tu ya tamaa ya mtu mmoja au wawili halafu Serikali inawafumbia
macho watu hawa kwakweli ni kitu ambacho kinasikitisha sana nakubaliana
kwamba Serikali nayo inashiriki“ — Mbunge Yusuph Salim.
“Wanaofanya
biashara ya dawa za kulevya sio wauza ndizi wala sio mtu mwenye mtaji
wa milioni tano wala kumi ni watu wenye hela nyingi, ndio maana hapa
kila mmoja anasema ana majina halafu anatetemeka kuwataja sababu anajua
akitoka tu hapa kichwa chake ni halali yao.
“Hivyo ndivyo ilivyo na alipokuwa anamalizia Kangi Lugola,
akawa anasema anaweza kuwataja hao watu ila hofu yani ni kuna watu
kulekule ndani anapowataja wanatoa siri kwamba aliyetuletea haya majina
ni Kangi Lugola.. hiyo ndio hofu iliyopo maana yake ni kwamba Serikali inashindwa kuwalinda wale wanaoleta hizo siri“–Mbunge David Silinde.
Bonyeza play kuwasikiliza Wabunge hao;
za play kuwasikiliza Wabunge hao;
1. Mbunge David Silinde
2. Mbunge Kangi Lugola
3. Mbunge Livingstone Lusinde
4. Mbunge Yusuph Salim


Note: Only a member of this blog may post a comment.