Wednesday, February 17, 2016

Anonymous

MBUNGE AVUNJA REKODI YA SHINDANO LA KUBUSU, BUSU LAKE LANASA KWA MKEWE MUDA MREFU HAIJAWAHI KUTOKEA


Mbunge Joseph Chinotimba Zimbabwe

Bwana Chinotimba na mkewe Vimbai
Mbunge mmoja nchini Zimbabwe Joseph Chinotimba ameingia katika kumbukumbu za Afrika baada ya kumbusu mke wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kunakiliwa barani Afrika. 
Mbunge huyo na mkewe walizoa tuzo hilo baada ya kupigana busu kwa dakika 10 na sekunde 17.
Rekodi hiyo iliwekwa katika hafla moja iliyopigiwa upatu na kunadiwa kuwa ''Mashindano ya busu refu zaidi kuwahi barani Afrika''

Hafla hiyo ilipangwa na kuandaliwa kwa ushirikiano na waandalizi wa Daftari la rekodi barani Afrika.
Hafla hiyo iliandaliwa katika mji mkuu wa Harare kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao iliyoadhimishwa jumapili.
Via>>BBC

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.