HII mpya! Kuna madai kwamba, kaburi la
aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Daudi Timoth
Ballali lililopo Makaburi ya Gate of Haeven (Geti la Mbinguni) Eneo Na.
6, Ploti Na. 241, Safu Na. 17 huko Maryland nchini Marekani lipo mbioni
kufukuliwa ili kuwezesha vipimo vya vinasaba (DNA) kutumika kwa lengo la
kubaini ukweli wa kifo chake, Ijumaa limeelezwa.
Gharama ya jumla ya kuwepo kwa kaburi
hilo ambalo safu yake imepewa jina la Jesus In The Temple (Yesu
Hekaluni) ni Dola za Marekani 4,800 (zaidi ya Sh. milioni 9 za
Tanzania).
Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa Ballali aishiye Bongo, familia inaona ni
vema kutimizwa kwa ombi hilo kwa vile manenomaneno kuhusu ‘Ballali kafa
au hajafa?’ hayajawahi kufunga breki tangu tangazo la kifo chake, Mei,
mwaka 2008.
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.
TWENDE PAMOJA
“Nadhani sisi familia hatuna umoja.
Wengine waoga, wengine majasiri. Lakini kwa sababu hata sisi hatukuwahi
kwenda Marekani kumzika ndugu yetu (Ballali), hivyo ili na sisi tuwe na
amani na kujua moja, tumetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwasiliana
na Marekani kwa lengo la kulifukua kaburi lake na kuutoa mwili.
“Hilo ni moja. Pili, mwili huo upimwe
DNA ili kubaini kama aliyezikwa ni Ballali? Hili zoezi halitatusaidia
sisi tu kama familia, lakini hata serikali yenyewe itakuwa na faida
maana maneno yamekuwa mengi sana. Tumeshaandaa utaratibu wa kuonana na
serikali kwa ajili ya kupanga hili,” alisema ndugu huyo akisisitiza
kusitiriwa kwa jina lake.
BALLALI FEKI AUMIZA KICHWA
Ndugu huyo aliendelea kusema kuwa, tangu
kifo cha Ballali, Mei, mwaka huo, Desemba posti ya kwanza ya mtu
aliyejiita Ballali ilitupiwa kwenye mitandao ya kijamii akisema
amekumbuka nyumbani Tanzania.
“Tangu wakati huo, mtu huyo amekuwa
akitupia maneno ya kushutumu kwamba yeye amefariki dunia. Hata vyombo
vya habari vya Tanzania vilipotembelea Marekani mwaka jana na
kuthibitisha kifo cha mchumi huyo kwa kuliona kaburi lake, mtu huyo
alisema anavishangaa vyombo hivyo kwa vile yeye yu hai.“Ndiyo maana
tunataka kaburi kufukuliwa, mwili utolewe na kufanyiwa vipimo mara moja
ili kuondoa utata huu,” alidai ndugu huyo.
Ndugu huyo alizidi kuweka bayana kuwa,
habari alizonazo ni kwamba, watoto wawili wa marehemu ambao alizaa na
mwanamke, raia wa Marekani wapo kwenye mchakato wa kutua Bongo wakati
wowote kwa mambo mawili makuu.
“Nasikia wanakuja. Lakini lengo la ujio wao ni kusema wanachokifahamu kuhusu kifo cha baba yao. Sasa sijajua watasema alifariki dunia au hajafariki dunia! Hiyo ni siri yao nzito, ipo mioyoni mwao.
“Lakini nijuavyo mimi kilio kikubwa cha hawa watoto mwaka ule wa tangazo la kifo kilikuwa ni kukosa kuiona sura ya baba yao wakati wa kuuaga mwili mpaka unaingizwa kaburini kwa mazishi.
“Nasikia wanakuja. Lakini lengo la ujio wao ni kusema wanachokifahamu kuhusu kifo cha baba yao. Sasa sijajua watasema alifariki dunia au hajafariki dunia! Hiyo ni siri yao nzito, ipo mioyoni mwao.
“Lakini nijuavyo mimi kilio kikubwa cha hawa watoto mwaka ule wa tangazo la kifo kilikuwa ni kukosa kuiona sura ya baba yao wakati wa kuuaga mwili mpaka unaingizwa kaburini kwa mazishi.
“Kingine wanafuatilia hisa. Baba yao
aliweka hisa kiasi cha shilingi bilioni 3 kwenye kampuni moja ya bia
Tanzania. Sasa kutokana na kusuasua kwa maelezo yasiyonyooka kuhusu
faida na hasara za hisa zile, ndiyo maana wanakuja. Nasikia tayari wana
mwanasheria kwa ajili ya kupata haki yao hiyo,” kilimalizia chanzo
hicho.
LOWASSA AOMBWA KUMLETA BALLALI
Katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 25, mwaka huu, mgombea wa urais kwa ‘leseni’ ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia mwavuli wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amekuwa akiombwa na wapiga kura wake
kumleta Ballali mara tu atakapoingia ikulu, jambo ambalo alikubaliana
nalo.
Lakini naye Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameibuka na kuonesha kushangazwa
na suala hilo kwani anachokijua kama waziri mwenye dhamana ni kwamba
Ballali alifariki dunia mwaka 2008

Note: Only a member of this blog may post a comment.