STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha jeuri
kwa kueleza kwamba anamlea mwanaye Terry kwa mapenzi tele ili
asimkumbuke baba yake, Dickson ambaye wamemwagana.
“Kama baba yake alikuwa akinipiga mbele yake au kuja akiwa amelewa tilalila unafikiri mtoto atamkumbuka? Nimelelewa na mama yangu na sikuwahi kumkumbuka baba mpaka hivi nimekuwa mtu mzima, kwa hiyo sioni shida kumlea mwanangu peke yangu, kila kukicha naongeza upendo kwake,” alisema Shamsa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.