Tuesday, June 2, 2015

Anonymous

PROF. MUHONGO ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

ALIYEKUWA Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani juu) naye ametangaza nia ya kuwania Urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa kwenye Ukumbi wa Chuo Huria huko Musoma mkoani Mara jioni hii. 

Prof. Muhongo amesema hawezi kutoa ahadi ya mishahara wakati hajakuza uchumi, hawezi kutoa ahadi ya kujenga shule wakati hajakuza uchumi hivyo atakuza kwanza uchumi kama ilivyo kauli mbiu yake ya 'Tukuze Uchumi, Tuondoe Umasikini.'
Katika hotuba yake, Prof. Muhongo amejikita sana katika takwimu na jinsi ya kuinua uchumi wa Taifa na kuondoa umasikini.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.