Brighton Masalu
Pombe zitamtoa roho! Unywaji wa
pombe kupita kiasi anaoufanya staa wa sinema za Kibongo, Blandina
William Chagula ‘Johari’ umetafsiriwa kama kujihatarisha kiafya baada ya
hivi karibuni kunaswa mchana wa jua la utosini akifakamia ulabu huku
akionekana kuzidiwa, jambo lililozua minong’ono kwa baadhi ya watu,
Risasi Mchanganyiko lilimnyatia.
Akiwa ‘ametumbua’ macho, mwandishi wetu alimfuatilia mhudumu huyo na kubaini kinywaji kilichoagizwa na Johari ni pombe ndipo akaweka sawa kamera yake kwa ajili ya lolote. Kwa kasi, paparazi wetu alimfotoa picha za mbali na kwa tahadhari ya kutoshtukiwa kabla ya kuondoka eneo la tukio.
Mwandishi wetu hakuweza kumfuata Johari mahali alipoketi na badala yake aliondoka kisha kumpigia simu ambapo awali alikataa kutokuwepo kwenye baa hiyo lakini baada ya kubanwa kwa hoja nzito, alijikuta akikiri na kufunguka jambo jipya.
“Dah! Ulikuwa umekaa wapi? Lakini siyo mawazo nimeamua tu kupumzika na kazi kwa leo hivyo nikaona si vibaya kama nitajiburudisha kwa kinywaji hiki,” alisema Johari.

Note: Only a member of this blog may post a comment.