Kama una mfollow Ben Pol kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii
sina shaka umeshakutana na picha akiwa ughaibuni, yuko nchini Ujerumani
na ameeleza kilichompeleka huko.
Hit Maker wa ‘Sofia’ Ben Pol amesema kuwa ameenda Ujerumani kushiriki
katika utengenezwaji wa video ya Mtanzania Emannuel Austin aishiye
huko, ambaye alimshirikisha Ben Pol kwenye wimbo wake alipotembelea
Tanzania mwaka jana.
“Kimsingi nipo nchini Ujerumani Frankfurt, niko na mshikaji wangu
mmoja anaitwa Emanuel Austin, ni choreographer ni muimbaji ambaye asili
yake ni Tanzania lakini yuko based nchini Ujerumani. Mwaka jana
alikuwepo Tanzania nilirekodi nae wimbo kwenye studio za Authentic,
lakini beat ilifanywa na Fundi Samweli. Kwahivyo sasa hivi tunafanya
music video huku Ujerumani tunafanya na the number one producer wa music
video huku Ujerumani.” Alisema Ben Pol kupitia 255 ya Clouds Fm.
Huu ndio wimbo wa Emanuel Austin na Ben Pol ‘Ruka Juu’
-via bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.