Monday, March 30, 2015

Anonymous

HATIMAYE KARDINALI PENGO AVUNJA UKIMYA...GWAJIMA AOMBA AOMBEWE!

Wakati hayo yakiendelea, jana Pengo aliwatangazia waumini wake kumsamehe Gwajima na pia kuwataka waumini wake pia wamsamehe.

Akizungumza katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph ambako iliendeshwa misa ya Jumapili ya Matawi, alitoa msamaha kwa Gwajima na kusema kuwa hana chuki na mtu yeyote.
Aidha, Pengo alisema hawezi kuingilia hatua ya Polisi kumhoji kiongozi huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Gwajima: Niombeeni
Aidha, katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Gwajima amewaomba waumini wake wamuombee kwa Mungu apone haraka ili aweze kuendelea na kazi aliyotumwa na Mungu ya kuhubiri Injili.


Taarifa iliyotolewa na kusomwa kanisani kwake imedai kuwa kiongozi huyo anaendelea vizuri na afya yake imeanza kuimarika. Alisema waumini wake wamuombee kwa Mungu apone haraka ili kuendelea na kazi aliyotumwa na Mungu ya kuhubiri injili.

Kiongozi huyo bado amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na anaendelea kupatiwa matibabu ya karibu na madaktari kutokana na hali yake kubadilika mara kwa mara.

Hata hivyo, kwa taarifa iliyotolewa na daktari anayemtibu askofu Gwajima, Fortunatus Mazigo, alisema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri japokuwa alikataa kusema ni nini tatizo linalomsumbua hadi akamilishe kukusanya taarifa ya vipimo vyote ambavyo vingine bado majibu yake hayajapatikana na huenda kila kitu kikawa hadharani leo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.